Madaktari Bingwa na Bobevu katika magonjwa ya Binadamu “MADAKTARI WA RAIS DKT. SAMIA” wamewasili leo Oktoba 28,2024, Wilaya ya Makete kwa ajili ya kutoa huduma za kitabibu kwa muda wa siku 5, kuanzaia Oktoba 28 hadi Novemba 1,2024.
Madaktari hao Bingwa wamebobea katika Magonjwa ya Wanawake na Ukunga, Watoto na Watoto Wachanga, Upasuaji katika Mfumo wa Mkojo, Usingizi na Ganzi, Kinywa na Meno, Mifupa na Ajali pamoja na Magonjwa ya ndani.