Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kifo cha mwanamke mmoja, Veronica Riwa (77), Mfugaji na mkazi wa Simbani wilaya ya Kibaha.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Muhudhwari Msuya ameeleza kuwa marehemu alikutwa nyumbani kwake akiwa ameuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa aliyefanya mauaji hayo ni mchungaji wa ng’ombe wa marehemu na baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea ili hatua za kisheria zichukuliwa dhidi yake” imesema taarifa ya Kaimu Kamanda Msuya
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa viongozi wa mitaa yao juu ya watu wanaoishi nao wakiwa ni wasaidizi wa kazi mbalimbali za nyumbani ili kusaidia kuwa tambura kirahisi yanapotokea matukio ya kijinai na kimaadili ili wachuliwe hatua stahiki.