Na; Henrick Idawa
Wazazi na walezi wa watoto walisajiliwa na kufadhiliwa na shirika la compassion International Tanzania kupitia kanisa la TAG Tandala la wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kuondokana na dhana potofu juu ya ufadhili huo kwamba unaweza kupelekea watoto kufundishwa maadili mabaya.
Akitoa elimu ya ufadhili huo
kwa wazazi na walezi Mratibu wa Mradi wa makuzi na malezi kwa watoto na vijana
Isaack Philipo amesema lengo kuu ni kuwalea watoto hao kwa muda wa miaka 22
katika malezi kimwili,kiroho kiuchumi na kijamii ili kuandaa kizazi bora na si
vinginevyo.
Amesema Mradi huo unalenga
Zaidi kwenye suala la ulinzi na usalamaa la mtoto hivyo wazazi waendelee kuwa
na Imani nao na kutambua kuwa watoto hao tangu sasa watashirikiana katika
malezi ikiwa ni sambamba nakujua kila hatua ya ukuaji wake kama watapatwa na
Tatizo lolote shirika nalo litawajibika kama mzazi wa mtoto.
Mchungaji Kiongozi wa kanisa
la TAG Tandala Jonas Sanga amesema ili kufikia malengo ya mradi huo na kuona
tija ni muhimu wazazi kuwalea watoto katika maadili mema kwani malengo ya mradi
nikuona watoto wanakua katika maadili mema.
'Ndugu zangu malengo ya mradi huu ni kuona mabadiliko kwa watoto wetu hivyo tusaidiane kuwafinyanga hawa watoto kutokaa katika malezi tuliyonayo kuwa katika malezi bora,vinginevyo mradi utakuwa haujasaidia' amesema Mch. Sanga
Mchungaji Sanga na Katibu wa
kamati ya mradi huo Peter msigwa wamesema ingekuwa mradi huo una malengo
tofauti na misingi ya Imani ya kanisa la Assembles of God TAG wasingekubalina
nao.
'Mnajua msimamo wangu kwa wale wanaonifahamu,mnajua msimamo wa kanisa hili na imani yetu,tusingekubali watoto hawa 200 kuwaingiza katika huko wanakosema tusingekubali,lakini niseme kama mtoto wako amesajiliwa hapa basi muwe na amani na sisi watoto wenu wako mikono salama' amesema Peter Msigwa
Kwa upande wa wazazi na walezi
Anitha Sanga na Venansia Ngulo wametoa shukrani zao kwa kanisa la TAG na
shirika hilo kwa kuwasaidia watoto wao na kwamba fedha mbazo zingetumika
kuwahudumia watoto hao sasa watazielekeza katika shughuli nyingine.
'kwa kweli tunashukuru kanisa la TAG na shirika hili kwa kutona maana maisha yetu ni ya kawaida na wakati mwingine watoto wetu wameishia mitaani kwa kushindwa kusomeshwa lakini kwa sasa watasomeshwa tunashukuru sana' wamesema wazazi
Ikumbukwe kuwa watoto 200
kutoka kijiji cha Tandala,Ikonda na ihela wananufaika na mradi huo ambao
inaelezwa wasomeshwa,kufadhiliwa matibabu muda wote, na wazazi kuepewa elimu na
mafunzo mbalimbali kama ya malezi na ujasiriamali ili wajiinue kiuchumi.Baada ya kikao wazazi na watoto wakapata chakula kilichoandaliwa na kanisa la TAG Tandala Wazazi na watoto wakipata chakula cha pamoja baada ya kikao octoba 26.2024
Mratibu wa mradi akitolea ufafanuzi kuhusu makubaliano ya kutoa au kutumia taarifa binafsi katika utekelezaji wa mradi pamoja na kuondoa zuio la kushtakiwa. |
Katibu wa kamati ya utekelezaji wa mradi huo kanisa la TAG Tandala akitoa neno katika kikao hicho Peter Msigwa |
Mratibu wa Mradi wa CIT kupitia kanisa la TAG Tandala akitoa ufafanuzi wa mradi kwa wazazi na walezi wanaonufaika na mradi huo |
Shuhuda na mmoja ya walionufaika na miradi ya Compassion International Tanzania CIT kutoka mkoa wa Iringa ambaye kwa sasa ni mwl wa shule ya sekondari Lupalilo. |
Mchungaji Kiongozi wa TAG Tandala akitoa somo kabla ya kuanza kwa kikao |
Dua ikifanyika kabla ya kuanza na kumaliza kikao na wazazi wa watoto katika kanisa la TAG octoba 26,2024 |