Rais Dkt.Samia ateua viongozi ,Mkeka huu hapa

Adimin
0

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 30,2024 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:



(i) Dkt. Leonard Douglas Akwilapo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Dkt. Akwilapo ni Katibu Mkuu Mstaafu, anachukua nafasi ya Prof. Penina Mlama ambaye amemaliza muda wake;

(ii) Prof. Zacharia Babubu Mganilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

Prof. Mganilwa ni Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), anachukua nafasi ya Dkt. Naomi Katunzi ambaye amemaliza muda wake;

(iii) Dkt. Mwamini Madhebehi Tulli ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA). Dkt. Tulli ameteuliwa kwa kipindi cha pili;

(iv) Mhandisi Dkt. Richard Joseph Masika ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Mhandisi Dkt. Masika anachukua nafasi ya Prof. Henry Mahoo ambaye amemaliza muda wake;

(v) Balozi Salome Thaddaus Sijaona ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU). Balozi Sijaona ameteuliwa kwa kipindi cha pili;

(vi) Prof. Joseph Nicolao Otieno ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala. Prof Otieno ni Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), anachukua nafasi ya Prof. Hamisi Malebo ambaye amemaliza muda wake;
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top