Jamii yapewa jukumu jipya na SHUJAAZ

Adimin
0

 Na Linda Akyoo-Siha

Wakati harakati za kumkomboa kijana wa Kike kiuchuni kwa njia ya ufugaji wa Kuku,Shirika la SHUJAAZ kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo imeitaka jamii kufanya mazungumzo na vijana wa kike wa Kitanzania ili kuweza kubainisha changamoto zinazo wakumba vijana hao katika ufugaji wa kuku na kutafuta suluhu za changamoto hizo.


Akizungumza wakati wa mafunzo hayo msimamizi wa Mradi wa "BINTI SHUJAAZ"   Bw.Lucky Komba ameziomba serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Maafisa mifugo wilaya,watendaji wa kata, vijiji, maafisa kilimo na ufugaji, viongozi wa kimila na viongozi wa kidini,kuwaskiliza mabinti wafugaji ili kubaini changamoto wanazopitia na kuweza kujuwa nikwa namna gani wanaweza kuwakomboa vijana wa kike wa Kitanzania wanaofuga kuku.


Hata hivyo mafunzo hayo yalifadhiliwa na shirika la mifugo na kilimo ambalo liliona umuhimu wa kutoa elimu kwa vijana wa kike kuhusu ufugaji bora wa kuku. Lengo la semina hiyo lilikuwa ni kuwapa wanawake vijana ujuzi na maarifa ya kutosha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kujipatia kipato cha ziada.

Aidha mnufaika wa elimu ya ufugaji wa kuku aliyopatiwa na SHUJAAZ Bi.Reyna Mrema mwanamke mahiri na mzoefu mkubwa katika ufugaji wa kuku. Aliwaeleza wanawake vijana kuhusu mbinu za kufuga kuku kwa njia bora na endelevu.Alisisitiza umuhimu wa kutunza kuku kwa afya na lishe bora, pamoja na umuhimu wa kufuga kuku kwa njia ya kisasa ili kupata mazao bora,na kuwahamasisha vijana kuingia kwenye fursa ya ufugaji Kuku na kuachana na dhana ya kuwekeza kwenye boda boda na bajaji.


Kwa upande wake Afisa Mifugo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Siha Bi.Conjesta Pastory ameishukuru taasisi ya SHUJAAZ kwa kushirikiana na ILR kwa kuweza kutoka mafunzo hayo kwa Wilaya ya hai kwani wameweza kuwafikia vijana wengi zaidi na kuwahasa vijana kuchangamkia fursa hiyo kwani inalipa.


Mafunzo hayo ni mwanzo tu wa safari ndefu ya mafanikio kwa wanawake vijana wa Kitanzania,katika Kijiji cha Ngarenairobi kilichopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro kwani Wameonyesha azma ya kupambana na changamoto zote za kiuchumi na kijamii ambazo zinaweza kuwakabili, na kusema kuwa wako tayari kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top