RC Mtaka akiri kuridhika na mradi wa ujenzi mabweni Wanging'ombe

Adimin
0

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, alifanya ziara ya ukaguzi  katika Shule ya Sekondari Wanging'ombe, ambapo alikagua ujenzi wa madarasa mapya na bweni la wasichana. Katika ziara hiyo, Mhe. Mtaka alieleza kuridhishwa kwake na kiwango cha ujenzi wa miradi hiyo na kuwapongeza wahusika kwa juhudi zao.


"Nimefurahishwa sana na kasi na ubora wa ujenzi wa madarasa haya pamoja na bweni la wasichana. Hii ni hatua kubwa katika kuhakikisha watoto wetu wanapata mazingira bora ya kujifunzia, na hakika miradi hii inakwenda kuboresha kwa kiasi kikubwa hali ya elimu hapa," alisema Mhe. Mtaka.

Mhe. Mtaka pia alitumia fursa hiyo kuzungumza na wanafunzi wa madarasa ya mtihani, akiwapongeza kwa juhudi zao za muda mrefu shuleni.

 Aliwahamasisha wanafunzi hao kuendelea na bidii katika masomo yao, akisisitiza umuhimu wa mitihani inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Nawapongeza kwa juhudi zenu na uvumilivu wenu katika masomo. Mtihani unaokuja ni nafasi yenu ya kuonesha kile mnachokijua, nawaomba mfanye vizuri, tumieni fursa hii kutokomeza ziro kabisa katika shule hii. Naamini mtafaulu na mtaleta heshima kwa shule yenu na jamii kwa ujumla," aliongeza.

Ziara ya Mhe. Mtaka inakuja wakati shule nyingi za Njombe zinaendelea na maandalizi ya mitihani ya kitaifa, huku Serikali ikitoa kipaumbele kwenye miundombinu bora ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora na mazingira mazuri ya kujifunzia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top