Mnyama aina ya simba ametajwa kuwepo wilayani Makete mkoani Njombe
Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Maliasili na Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete Upendo Mgaya katika kikao cha baraza la Madiwani la halmashauri hiyo kilichoketi leo Novemba 7,2024.
Mgaya amesema nyayo za mnyama huyo zimeonekana katika maeneo tofauti ya Kata ya Iwawa hasa maeneo ilipo shule ya msingi St Joakim.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hawa Kader wametaka wananchi kuchukua tahadhari juu ya mnyama huyo.
Hii ni mara ya pili kwa kipindi cha miezi miwili tangu kuripotiwa nyayo za mnyama simba katika kata ya Lupila,mbalate na Mang'oto ambaye hata hivyo ilielezwa ameuawa katika wilaya ya Ludewa.