Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi Makete watakiwa kufuata Kanuni za Uchaguzi

Adimin
0

 Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Makete, Ndg. William M. Makufwe, amewataka wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Makarani kuhakikisaha kuwa wanafuata Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Mitaa, ngazi ya Vijiji na Vitongoji utakaofanyika Novemba 27,2024 siku ya Jumatano.


Ndg. Makufwe, amesema hayo Novemba 23,2024 wakati akizungumza na Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi pamoja na Makarani kwenye Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kusimamia vituo vya uchaguzi kwa Kanda ya Mfumbi.

“ikiwa utapata changamoto yoyote katika zoezi la uchaguzi utakaofanyika Novemba 27,2024, hakikisha kuwa unawasiliana na mtu sahihi ambaye atakuwa mtatuzi wa changamoto hiyo” Alisema Makufwe.

Aidha, Ndg. Makufwe, amewataka Wasimamizi wa Vituo pamoja na Makarani kuhakikisha kuwa wanawahi kwenye vituo vyao ambavyo wamepangiwa kusimamia siku hiyo ya uchaguzi ili kuweka mazingira sawa, yatakayo wawezesha kufanya kazi kiuweledi.

Sambamba na hayo, Ndg. Makufwe, amesema kuwa, kila mtu awajibike kwa nafasi yake ikiwa ni pamoja na kufuata maadili ya kazi, katika utekelezaji wa majukumu yao katika usimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ifikapo Novemba 27,2024.

Katika hatua nyingine, Wasimamizi hao wa Vituo vya Uchaguzi, pamoja na Makarani, wameapishwa Kiapo cha Uaminifu na Kutunza Siri panoja Kiapo cha Utii na Uadilifu, chini ya Kanuni ya 48 ya kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za Mwaka 2024.

Ikumbukwe kuwa, Mafunzo hayo ya Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia kura pamoja na Makarani yamefanyika leo Novemba 23,2024, ambapo kwa Wilaya ya Makete, kumekuwa na Kanda saba za Lupila, Ipepo, Tandala, Mfumbi, Bulongwa, Iwawa na Ikuwo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top