Mwanaume Makoye Peter Mayala (45) wa mkoani Shinyanga amejinyonga baada ya kumjeruhi mtoto wake na kitu chenye ncha kali Anna Makoye (06) anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mwamagunguli.
Tukio hilo limetokea alfajiri ya Desemba 2, 2024 baada ya marehemu kutokuwa na maelewano na mkewe Elizabeth Mwigulu ndipo mkewe aliamua kukimbia na marehemu kuamua kumjeruhi vibaya mwanaye maeneo ya shingoni na kisha kujinyonga huku chanzo kikiwa bado hakijajulikana.
Jeshi la polisi mkoani shinyanga limefika eneo la tulio kwaajili ya kufanya uchunguzi wa awali na kuzingumza na wananchi wa eneo hilo na kutoa rai kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi pindi wanapokumbana na changamoto za kifamilia.