Kwa mujibu wa taarifa kutoka @mn_boxing_tanzania_page Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Abbasi Mselemu afariki dunia alipokuwa kwenye majukumu ya kazi visiwani Zanzibar.
Tarehe 30/11/2024 Marehemu bondia Mselemu alipanda uliongoni kwenye Mapambano ya Usiku Wa Left Hook Ya Baba Mwinyi yaliyoandaliwa na Machatu Boxing Promotion huku yakifanyika kwenye ukumbi Zanzibar Golf Club Visiwani Zanzibar.
Marehemu Mselemu alicheza pambano la utangulizi la raundi 6 dhidi ya bondia Bakari H Bakari mkazi wa huko huko Visiwani Zanzibar pambano ambalo Mselemu alidondoshwa kwa TKO kwenye raundi ya 6.
Baada ya tukio hilo wakati wanatangaza matokeo ya mshindi wa pambano hilo Marehemu Mselemu alikaa chini na kulala kwenye sakafu ya ulingo na kupoteza fahamu ndipo taratibu za haraka zikafanyika kumuwahisha Hospital ya Mnazi Mmoja.
Na kwa mujibu wa mtu aliyekuwa karibu na Marehemu alisema kuwa Marehemu Mselemu kutokana na vipimo vilivyofanyika hospital hapo alitakiwa kufanyiwa upasuaji kabidi wamuache kwenye hospital hiyo ambako siku ya jana ya majira ya saa 12 jioni ndipo alipopatwa umauti.
Mwili wa Marehemu Abbasi Mselemu umesafirishwa asubuhi ya leo na utawasili jijini Dar es salaam ambapo utafikishwa kwa familia yake kwaajili ya taratibu za mazishi maeneo ya Mwinyi Mkuu Magomeni na kwa taarifa tulizokuwa nazo bondia huyo atasafirishwa kwenda kuzikwa mkoani Morogoro siku ya kesho.
Mn boxing inatoa pole kwa familia ya Marehemu bondia Abbasi Mselemu na wanafamilia wote wa mchezo wa masumbwi wa msiba huo mzito
Hiyo ni taarifa kutoka @mn_ boxing_ mtanzania_page ambayo waliiposta kwenye page yao