Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na mabadiliko ya Viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na mabadiliko ya viongozi hao ni kama ifuatavyo:-
Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi;
Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;
Bw. Gerson Msigwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali;
Dkt. James Henry Kilabuko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu);
Dkt. Stephen Justice Nindi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji;
Dkt. Suleiman Hassan Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara.
Aidha, Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene atapangiwa kituo cha kazi;
Prof Mohamed Yakub Janabi ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Afya na Tiba. Aidha, pamoja na nafasi hiyo Prof. Janabi ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili;
Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;
Bw. Mobhare Matinyi ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;
Kamishna wa Polisi CP. Suzan Kaganda ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi; na
Bw. Thobias Makoba aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi.
Uapisho wa Viongozi walioteuliwa utafanyika Ikulu Ndogo, Tunguu Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024 kuanzia saa 5.00 asubuhi.