Katika kusherekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya Kituo cha Malezi na Makuzi kwa watoto na Vijana TAG Tandala kwa kushirikiana na Shirika la Compassion Internation Tanzania wananchi wamekumbushwa kutenda matendo ya huruma kwa wengine ikiwa ni kutekeleza amri iliyo kuu ya Upendo.
Akizungumza Mratibu wa Mradi wa watoto na vijana Isack Filipho wa Kituo hicho amesema shirika la Compation International Tanzania limetoa zawadi ya nguo kwa lengo la kufanya matendo ya huruma kwa wengine na ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa malezi kwa watoto na vijana ambao umeanza hivi karibu kuwahudumia watoto 198 kati ya 200 walioandikishwa.
Isack amesema kila mtoto wa kike amepata gauni, nguo ya ndani na soksi huku mtoto wa kiume akipata Suruali ,shati/t-shirt na soksi nguo za dukani fashion ya kisasa na kwa kuzingatia size ya mtoto husika.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa kamati ya kituo hicho Maulisia Sanga amesema Malengo ya kituo hicho nikuwalea watoto katika misingi ya maadili na kiimani ili kuanda kizazi bora cha baadae kwa ushirikiano wa kanisa na wazazi.
Makamu Askofu wa TAG Mkoa wa Njombe Mch. Joseph Kipukapuka amesema wazazi wanalojukumu kubwa la kuhakikisha wanalea watoto wao katika maadili,kiimani ili kuandaa kizai bora cha baadae.
Kwa upande wake mwakilishi wa Jeshi la Polisi Kituo cha Polisi Tandala na Mchungaji Kiongozi wa TAG Tandala wamekemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwatendea vitendo vya ukatili watoto na kwamba ukibainisha sheria itachukua mkondo wake.
Akizungumza Mgeni Rasmi katika sherehe za kugawa Zawadi kwa watoto wanaonufaika na mradi wa malezi kwa watoto na Vijana TAG Tandala Diwani wa kata ya Tandala Daniel Hatanaka amesema watu waelewe kuwa huduma hiyo ni kutenda matendo ya huduma kwa wengine wasibabaishwe na jina la Compassion International Tanzania.
'Mratibu wasaidie hawa watu kuelewa hii huduma ukienda maeneo mengine kama Dodoma hili shirika wanalifahamu toka siku nyingi halijaanz akufanya kazi leo huku Makete ndio huduma imeingia ,wajue mwanzilishi alitenda matendo ya huruma kwa wengine hivyo hata sisi tujifunze kutenda matendo ya huruma kwa wengine na hata bibilia ndio inasema amri iliyokuu ni Upendo,upendo ni kuwajali wengine' amesema Hatanaka.
Kanisa la TAG limesema kuanzia Januari Watoto hao 200 wanatarajiwa kuanza kugharamiwa masomo na mahitaji mengine mbalimbali huku likitarajiwa watoto wanaonufaika na wasionufaika kuwaanzishia shule ya awali ili kuwalea katika maadili mema na kwa ukaribu zaidi.