Kanisa la TAG Tandala lililopo wilayani Makete Mkoani Njombe limesema linaungana na serikali katika kampeni mbalimbali ikiwemo za kukemea vitendo vya Ukatili pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuzingatia Mlo kamili.
Mchungaji Jonas SANGA Akisoma waraka huo Kupitia IDAWA MEDIA |
Kauli hiyo imetolewa na Mch. Jonas Sanga wa Kanisa la TAG Tandala mara baada ya kusoma waraka wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe uliotolewa Disemba 24,2024 ambao uliwataka viongozi wa dini kutumia siku za Ibada za sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kusoma waraka huo wenye lengo la kutoa elimu na kukemea vitendo vya ukatili na mauaji mkoani Njombe.
Mchungaji sanga amesema suala la Njombe kuendelea kuwa na
kiwango kikubwa cha watoto wenye udumavu ni aibu kwani imejaliwa kuwa na ustawi
wa ina mbalimbali wa mazao ukilinganisha na maeneo mengine ambayo hayana ustawi
mzuri wa mazao.
'Ukipita maeneo ya Dodoma,Iringa kwenda Dar mikoa ya Singida kuna maeneo mpaka unajiuliza hivi watu wa huku wanaishije,maana unaona dalili za ukijali mpaka masiki na wakati mwingine ni miezi michache lakini sisi njombe mpaka Makete kijani muda wote' amesema Mch. Sanga
Amesema moja ya kauli iliyomvutia ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwamba hata ukipanda kidole kinaota Njombe kwa maana kuwa mbegu yoyote itakayopandwa kwa mkono eneo lolote mkoa wa Njombe itastawi hivyo kila mmoja ahakikishe anakula mlo kamili.
Sanga amewataka waumini kutambua kuwa kumshibisha mtoto na kujaza tumbo sio lishe badala yake mtoto ale kwa kiasi kwa mchanganyo wa vyakula mbalimbali kila apatapo mlo.
Kuhusu vitendo vya Ukatili ikiwemo mauaji ya ndoa na
yanayohusishwa na imani za ushirikiana ili kupata Utajiri Mchungaji amewataka
waumini kutambua fedha na dhahabu ni mali ya Bwana hivyo wakimshirikisha Mungu
watafanikiwa kuwa na mali halali bila kuumiza wengine.
Bibilia inakataza masuala ya ukatili,tuishi kwa kupendana kama ni mali utaipata kw akufanya kazi kwa bidhii na kumtumaini Mungu muda wote na kumbuka Bibilia inasema fedha na dhahabu ni mali yake Bwana hivyo sio mpaka utoe kafara ya ndugu yako kwa kwenda kwa waganga huko!.
Amesema Waumini wanaposherekea sikukuu ya Krsimasi waumini wakumbuke kumuomba Mungu na kuacha kufanyiana vitu vya ajali vinavyohusisha ushirikina na mali za kafara kwani Dini na serikali inakataza mambo hayo na kwamba ni dhambi na kosa mbele ya sheria za Nchi.
Akishiriki Ibada ya Krismasi Disema 25 mwaka Jimbo la Kanisa
Katoliki Njombe Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema lengo la Waraka Huo
ni kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya masuala ya ukatili na lishe.
Akiongea na waandishi wa habari nje ya Kanisa hilo amesema serikali inatumia kila jukwaa la mikusanyiko ya watu kufikisha elimu ili mkoa wa Njombe ukomeshe vitendo vya ukatili na mauji sambamba na kuhakikisha watoto wanaupata lishe bora na kuepukana na Udumavu.