Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, uhamisho na mabadiliko ya viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka uteuzi, uhamisho na mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:
a) Wakuu wa Wilaya
(i) Bw. Godfrey Eliakimu Mnzava, Afisa Tarafa ya Ilemela ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. James Wilbert Kaji aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);
(ii) Bw. Michael John Semindu, Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu kuchukua nafasi ya Bi. Veronica Arbogast Kessy ambaye amestaafu;
(iii) Bw. Khamana Juma Simba, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga kuchukua nafasi ya Dkt. Julius Keneth Ningu ambaye amestaafu;
(iv) Bw. Hamad Rajabu Mbega, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi;
(v) Bw. Peter Nicholaus Masindi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu;