Mkurugenzi Kashushura atoa rai kwa watoa huduma za afya

Adimin
0

Na Stephano Mango, Mbinga 

MKURUGENZI  Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura  amewataka watoa huduma wa  Kituo cha Afya Matiri  kutoa huduma bora za afya huku akisisitiza kuwa  ongezeko la  watoa huduma   kituoni hapo liendane na utolewaji wa huduma bora za afya.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura akizungumza na Wataalam wa Sekta ya Afya


Hii ni baada ya Serikali kuajiri watoa huduma za afya  nchini hivi karibuni  na Halmashauri  ya Wilaya ya Mbinga kuwa mnufaika wa ajira hizo.


Mkurugenzi Kashushura ametoa rai hiyo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea kituo cha afya Matiri kilichopo Halmashauri  ya Wilaya ya Mbinga.


" Jumla ya watumishi nane wameongezeka hapa sasa kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha analeta tija kwa jamiii,  hakikisheni mnafanya  kazi kwa weledi" Amebainisha



Kwa upande wake Katibu wa Afya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga  George Mhina ameeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepokea jumla ya Watumishi 81 wa kada ya afya na Kituo cha Afya Matiri kimepokea watumishi 8.


Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Matiri  William Mbwambo amebainisha kuwa ongezeko la watoa huduma limeleta tija kwa wananchi wa Matiri ambao awali walilazimika kwenda katika vituo vya afya binafsi au  vilivyopo nje ya Kata hiyo jambo ambalo liliwaongezea gharama.


Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo Jane Zackaria  ameeleza kuwa  awali kituo kilihudumia  wagonjwa wapatao 400 kwa mwezi lakini sasa Kituo kinahudumia wagonjwa zaidi ya 600.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top