Mkurugenzi Makufwe awaaga rasmi Wanamakete

Adimin
0

 Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Ndg. William M. Makufwe,  Februari 11,2025, amekabidhi Ofisi kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. Jerry Daimon Mwaga, mara baada ya Watendaji hao kuhamishwa kwenye Vituo vyao vya kazi vya awali.


Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mhe. Christopher Yonam Fungo, amemtakia heri Ndg. Makufwe katika kituo chake kipya cha Kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.

Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. William Mathew Makufwe, amewashukuru watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kwa kuwa na ushirikiano mzuri kwa kipindi chote ambacho amekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.

Sambamba na hayo, Ndg. Makufwe, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kumuamini na kumhamishia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. Jerry Daimon Mwaga, amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo, kuendelea kuonesha mshikamano pamoja na Utendaji Mzuri uliotukuka kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.


Ndg. Jerry, ameongeza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kwa kuendelea kumuamini na kumhamishia katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete, na kuahidi kuendeleza mazuri ya Ndg. Makufwe ikiwa ni pamoja na Miradi Mkakati.

Ikumbukwe kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mwishoni mwa mwezi wa kwanza alifanya mabadiliko ya Viongozi mbalimbali wakiwemo wakurugenzi Watendaji wa Halamashauri, Wakuu wa Wilaya na Katibu Tawala
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top