Naibu Waziri Mkuu ataka raslimali zetu zitumike kuzalisha Umeme

Adimin
0

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa pamoja na dunia sasa kuweka mkazo ikiwemo ya kifedha kwenye uzalishaji umeme kwa kutumia nishati jadidifu kama vile jua, maji na upepo,  nchi za Afrika zinapaswa kutumia vyanzo ilivyonavyo kama vile makaa ya mawe ili kuweza kuwa na umeme wa kutosha.



Dkt. Biteko amesema hayo   Februari 11, 2025, New Delhi, India wakati akishiriki katika mjadala wa Mawaziri wa Sekta ya Nishati kutoka India, Qatar, Uingereza na Tanzania wenye  mada iliyosema Mpango Mpya wa Dunia wa Biashara ya Nishati ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Wiki ya Nishati India.

Dkt.Biteko ametolea mfano kuwa Tanzania ina madini ya makaa ya mawe ya kutosha pamoja na urani ambayo yanafaa kuzalisha umeme hata hivyo kumekuwa na changamoto ya kupata ufadhili wa kuyaendeleza kwa  ajili ya kuzalisha umeme kwa vile yanatajwa kusababisha uchafuzi wa mazingira akieleza kuwa makaa ya mawe yanaweza kutumika kuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye kuondoa sumu ya kaboni.

Amesema kuwa takribani watu milioni 600 barani Afrika hawajafikiwa na huduma ya umeme hivyo kwa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo makaa ya mawe itawezesha lengo la kufikishia umeme watu hao kwa haraka.

“ Afrika inachangia  uchafuzi wa mazingira kwa kiasi  kidogo kwa sababu ni bara maskini lakini inatajwa kuwa na mchango sawa na mataifa mengine, mabadiliko ya matumizi ya nishati hayakwepeki, nchi ziruhusiwe kuwa na uendelezaji endelevu wa rasilimali zake kwa ajili ya kuwa na usalama  wa nishati.” amesisitiza Dkt. Biteko.


Ameongeza “ Lazima tuangalie ukweli na hali halisi mfano Qatar au India hali yao ya upatikanaji umeme ni tofauti na Tanzania,  hatutaweza kutumia njia ya aina moja kwa ajili ya kutatua changamoto za masuala ya umeme kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea ni lazima kutumia njia tofauti,”

Ameangazia lengo la Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi Afrika (Mission 300) uliofanyika nchini Tanzania hivi karibuni wa kufikisha nishati ya umeme kwa watu milioni 300 barani humo ifikapo mwaka 2030
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top