Mwalimu Mkuu wa shule adaiwa kujinyonga kwa sumu Mkoani Shinyanga

Adimin
0

 Mkuu wa shule ya sekondari Chambo iliyopo katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, Zaharani Patrombeyi (44), amejiua baada ya kunywa kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo SACP Janeth Magomi, amethibitisha kwa njia ya simu kutokea kwa tukio hilo na kwamba jaribio la kunywa kimiminika hicho lilifanyika January 29 mwaka huu 2025, majira ya saa tano asubuhi katika kijiji na kata Chambo, tarafa ya Dakama.

SACP Magomi alieleza kuwa baada ya Mwalimu huyo kunywa kimiminika kinachosadikiwa kuwa ni sumu alizidiwa na ndipo alipokimbizwa katika hospitali ya manispaa ya Kahama kwa matibabu ambapo alipoteza maisha January 31 majira ya asubuhi wakati akiendelea na matibabu.

Alisema kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kujua chanzo cha Mwalimu huyo kufikia hatua hiyo kwani hakuacha ujumbe wowote kuhusiana na tukio hilo.
“Alijaribu kujiua kwa kunywa kitu kinachosadikika kuwa ni sumu ambacho bado tunasubiri uchunguzi wa daktari, na kwa bahati mbaya sana majira ya asubuhi Mwalimu huyo amefariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kahama” Alieleza Kamanda Magomi

Alieleza kuwa jaribio la kujiua ni kujichukulia sheria mkononi na endapo Mwalimu huyo asingefariki basi angeshtakiwa kwa kujaribu kujiua ambalo ni kosa kisheria.

Mmoja wa mashuhuda ambae hakutaka kutaja jina lake, alisema Mwalimu Zaharani enzi za uhai wake hakuwahi kuwa na ugomvi na mtu yeyote, kijijini hapo, alishirikiana vyema na jamii inayozungumka, na kwamba hata wao wameshangaa kuona akiwa katika hali mbaya akipelekwa hospitalini na mwisho wake kufariki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top