Sai mbaroni kwa kuiba mtoto,Polisi watoa taaarifa hii

Adimin
0

 Jeshi la Polisi mkoani wa Shinyanga linamshikilia mwanamke mmoja mkazi wa kata ya Mwakitolyo Sai Charles (38) kwa tuhuma za kuiba mtoto wa siku moja wa Rahel Mathayo (19) mkazi wa kijiji cha Bulige kata ya Bulige wilayani Kahama.


Akizungumza na Wasafi Media Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga SACP. Janeth Magomi, amesema tukio hilo lilitokea Februari 5, 2025 majira ya saa 1:00 asubuhi katika kijiji cha Bulige ambapo mama wa mtoto huyo hakumuona mwanaye alipotoka kuoga mara baada ya kumuamini mtu baki aliyemsindikiza nyumbani mara tu alipojifungua.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Magomi baada ya kugundua kuwa mtoto wake ameibiwa, alipiga kelele na kuomba msaada ambapo vijana wa bodaboda waliokuwa karibu walitoa taarifa kwa jeshi la polisi, wakieleza kuwa mtuhumiwa alikuwa amepanda pikipiki akiwa na mtoto mdogo ndipo Jeshi la Polisi lilifanya msako wa haraka na kufanikiwa kumkamata Sai Charles akiwa kata ya Mwakitolyo na mtoto huyo ambaye tayari amerudishwa kwa mama yake mzazi.

Kamanda Magomi amewataka wananchi hasa wanawake kuwa makini na watu wanaojitokeza kama ndugu au marafiki baada ya kujifungua kufuatia uwepo wa matukio mengi ya wizi wa watoto na kutoa rai kwa wananchi kuwa wizi wa watoto ni kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya aina hiyo.

Nao baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wametoa maoni yao juu ya vitendo vya wizi wa watoto huku wakiiomba serikali kupitia mamlaka zinazohusika kuwachukulia sheria kali wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Mpaka sasa mtuhumiwa Sai Charles anashikiliwa na Jeshi la Polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top