Jamaa akatwa korodani na mwajiri wake kisa kudai pesa yake

Adimin
0

 Mwanamume wa umri wa makamo anaendelea kupata nafuu katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kirinyaga baada ya kufanyiwa upasuaji wa sehemu za siri kufuatia shambulio la kinyama lililofanywa na mchinjaji, anayedaiwa kuwa mwajiri wake.


Alifichua kuwa shambulio hilo lilitokea, Februari 7,2025 alipoenda kudai salio la KSh 50 kutoka kwa mwajiri wake aliyetambuliwa kama Isaac Gachoka. 

Kulingana na Muthii, Gachoka alimkokota kwa nguvu hadi chumbani kabla ya kumpiga na kumkata sehemu zake za siri.

 "Alinivuta ndani kwa nguvu na kuanza kunijeruhi sehemu ya chini ya mwili wangu hadi kila kitu kilikatwa," Muthii alisimulia kwa uchungu.

 Muuguzi katika hospitali hiyo alielezea ukali wa majeraha aliyopata Muthii, akieleza kuwa kifuko chake cha  korodani kilikatwa, alithibitisha kuwa timu ya matibabu ilifanikiwa kurekebisha uharibifu.

“Alifika kituoni akiwa na majeraha makubwa. Baada ya upasuaji, tulifanikiwa kuunda upya mfuko wa ngozi kwa wakati, na sehemu zake za siri sasa ziko salama," alisema. 

Licha ya kunusurika katika shambulio hilo baya, Muthii sasa anakabiliwa na changamoto nyingine—kumaliza bili yake ya hospitali.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top