Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Chiku Abdallah Ally (33), mkazi wa Sokoine- Mvomero kwa tuhuma za kumjeruhi mume wake.
Tukio hilo limetokea Machi 3, 2023, ambapo mtuhumiwa alimjeruhi mume wake Andrea Mhangai Madila, (52) mkulima na mkazi wa kijiji cha Wami Sokoine kwa kutumia silaha yenye ncha kali kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili, hali iliyomsababishia majeraha na damu kuvuja kwa wingi.
Majeruhi amelazwa Hospital ya Wilaya ya Mvomero akiendelea na matibabu.
Jeshi la Polisi limesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliotokana na vitendo vya ukatili na dhuluma kwenye familia yao.