Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amempangia Balozi Mobhare Holmes Matinyi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.
Rais Samia amempangia pia Balozi Hamad Khamis Hamad kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji na amemteua pia Dkt. Rachel Stephen Kasanda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi akichukua nafasi ya Lauteri John Kanoni ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Rais Samia amemteua pia Prof. Jafari Ramadhani Kideghesho kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania na amemteua CPA. Ashraph Yusuph Abdulkarim kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo.