BBT yawafikia Wananchi Makete ,DC Awafikishia salaam wananchi

Adimin
0

 Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Kissa Kasongwa, amewataka vijana na wanawake wa Wilaya hiyo kuchangamkia fursa ya uwepo wa Mradi mkubwa wa Kilimo wa BBT, “Building Better Tomorrow”, kutokana na umuhimu wake katika kujenga uchumi wa nchi pamoja na wakazi wa eneo hilo kiujumla.


Mhe, Kasongwa amesema hayo, Mei 26,2025, akiwa kwenye mkutano wa Hadhara na wakazi wa Kata ya Kinyika katika kijiji cha Nungu, mara baada ya kukagua Shamba ambalo litatumika katika Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora, BBT, kwa wakazi wa eneo hilo.

“Niipongeze sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Kilimo kwa kuanzisha BBT ambayo imekuwa mkombozi kwa vijana wengi, sambamba na kufanya ukaguzi wa eneo la Ekarii 100, na kutoa elimu kwa Wananchi juu ya malengo ya BBT, ambapo Programu hiyo itakwenda kuwa chachu ya mabadilikoya kiuchumi” alisema Mhe. Kasongwa.

Aidha Mhe. Kissa, ameongeza kuwa, kupitia BBT, Makete itakwenda kuzalisha mazao yenye tija kwa kuwa kuna rasilimali watu ya kutosha na kwamba wanaenda kuanzisha kilimo Biashara ili kutimiza adhima ya maono ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ya kuchangia asilimia 10 kupitia sekta hiyo muhimu ifikapo mwaka 2030 kupitia Agenda 10/30.

Kwa upande wake, Mhandisi Anitha James kutoka Wizara ya Kilimo, amesema kuwa Programu hiyo itakwenda kuchochea uzalishaji wenye tija na kupatikana kwa masoko ya uhakika kwa vijana na wanawake watakaonufaika na Programu hiyo ya BBT, na ametoa rai kwa Wananchi wa wilaya ya Makete ambao ni vijana na Wanawake kuchangamkia fursa hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wanananchi wa kijiji cha Nungu, Mwenyeketi wa kijiji hicho Bw. Essau Ndaga ameipongeza Serikali kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Programu ya BBT, ambapo itakwenda kuchochea maendeleo katika sekta ya Kilimo na kama kijiji kitatoa ushirikiano kwa waratibu wa Programu hiyo.

Ikumbukwe kuwa, Ukaguzi wa shamba na utoaji wa Elimu juu ya Programu hiyo kwa Wananchi umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Kissa Kasongwa pamoja na Mhandisi Anitha James ambaye ni Mratibu wa BBT ngazi ya Halmashauri kutoka Wizara ya Kilimo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top