Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, ameibuka na kukemea vikali vitendo vya utekaji vinavyoendelea kuripotiwa nchini Tanzania, akitaka uwajibikaji wa Waziri wa Mambo ya Ndani na kusisitiza kuwa viongozi wote lazima wakosolewe wanapokosea, bila kujali nafasi zao.
Akizungumza mbele ya wakazi wa Mwabuma, jimboni Kisesa mkoani Simiyu, Mpina amesisitiza kuwa kutojali au kuoneana aibu katika kukosoana kumechangia kuzorotesha uwajibikaji serikalini na kuwaumiza wananchi.
Mbunge huyo alimrejea Padri Charles Kitima, aliyeshambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa "wasiojulikana", akisema tukio hilo ni mfano wa namna hali ilivyofikia pabaya na kwamba haiwezekani Waziri mwenye dhamana aendelee kushikilia ofisi huku watu wakiumizwa hadharani.
TAZAMA FULL VIDEO ON YOUTUBE👇👇
Mpina amesisitiza kuwa viongozi wote kuanzia ngazi ya chini hadi juu, wakiwemo mawaziri, wabunge, madiwani hata Rais, wanapaswa kukosolewa kwa mujibu wa Katiba, na kwamba kila Mtanzania ana haki ya kuishauri au kuikosoa serikali bila kuzuiwa.