Chama cha Mapinduzi (CCM @ccm_tanzania) kimesema uchaguzi hauwezi kusogezwa mbele kwani wamejipanga kushiriki uchaguzi na hawawezi kuwa sehemu ya kuvunja Katiba, hivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA @ChademaTZ2) wajipange 2030
Katibu NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makalla ameeleza hayo Mei 15.2025 wakati akizungumza na wananchi wa majimbo la Kilosa na Mikumi katika wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro akimalizia ziara yake ya siku saba (7) iliyokatishwa kupisha maombolezo ya msiba wa Hayati Cleopa David Msuya
CPA Makalla amesema hakuna jambo la dharura wala vita la kufanya uchaguzi uhairishwe na wala nchi haipo kwenye vita wala jambo lolote la kutisha kusema uchaguzi ushindwe kufanyika
Amesema CCM ni chama kinachoheshimu demokrasia na hawapo tayari kuvunja Katiba na kwakuwa CHADEMA hawashiriki uchaguzi wasubiri 2030
“Wenzetu hawa nimesikia walianza juzi Bukoba, Geita, wameenda Mwanza nikasikia Myika na Heche wanasema tunaomba uchaguzi usogezwe mbele mpaka tufanye mabadiliko, hakuna mwenye mamlaka ya kusogeza uchaguzi, uchaguzi upo kwa takwa la Kikatiba na mimi nawaambia Mnyika na Heche tuko tayari kwa uchaguzi, sijui wako wapi?, ACT wameanza kuchukua fomu na sisi tumejipanga kwenye chama chetu tunaenda kwenye uchaguzi” -CPA Makalla