Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho na uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uhamisho na uteuzi huo ni kama ifuatavyo:
Mhe. Albert Gasper Msando amehamishwa kutoka Wilaya ya Handeni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo;
Mhe. Japhari Mghamba Kubecha amehamishwa kutoka Wilaya ya Tanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni;
Mhe. Dadi Horace Kolimba amehamishwa kutoka Wilaya ya Karatu kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga;
Bw. Lameck Karanga Nganga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Nganga alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu;
Bw. Bahati Migiri Mfungo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mfungo alikuwa Afisa Tarafa ya Mbuguni, Wilayani Arumeru;
Bw. Lazaro Jacob Twange ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Twange alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo; na
(vii) Bw. Andrew William Massawe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). Bw. Massawe anachukua nafasi ya Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman ambaye amemaliza muda wake.