Taarifa Mpya kuhusu Tundu Lissu, Sasa kufikishwa Mahakamani

Adimin
0

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka Upande wa Serikali kukamilisha upelelezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.


Kesi hiyo ya uhaini imetajwa mei 6,2025 mbele ya Hakimu Mfawidhi, Franko Kiswaga ambaye ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 19, 2025 huku akiutaka Upande wa Serikali kukamilisha upelelezi.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tawabu Issa alieleza mahakama hiyo kwamba shauri limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika, lakini pia mshtakiwa Lissu amegoma kushiriki kesi hiyo kwa njia ya mtandao kutokea gereza la Ukonga.

Kwa upande wake, Juma Mwaibako ambaye ni Mkuu wa Gereza la Ukonga amedai kuwa mtuhumiwa amekataa kusikiliza shauri hilo na kupanda mahakamani.

Madai ya kutokamilika kwa upelelezi yalipingwa vikali na Jopo la Mawakili wa Utetezi wakiongozwa na Mpale Mpoki aliyesema kwamba haoni sababu ya upelelezi kutokamilika kwa muds mrefu takribani siku 27.

“Nashangaa kwa nini upelelezi haujakamilika, sioni kwenye hati ya mashtaka, tuambiwe ni kitu gani kinachoendelea.”

Wakili Tawabu alidai kuwa wanaandaa nyaraka na zikikamilika watazipandisha mahakamani lakini hakuna sheria inayowalazimisha kusema lini watakamilisha upelelezi.

Mahakama imetoa amri ya Tundu lissu kupelekwa mahakamani siku ya kesi yake ikiwa ni sambamba na kuruhusiwa kwa watu kuhudhuria kusikiliza kesi hiyo itakayoendeshwa kwa uwazi.

Lissu alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Aprili 10, 2025 akikabiliwa na kesi mbili za jinai ikiwemo uhaini na kuchapisha taarifa za uongo ambayo alisomewa mbele ya mahakimu wawili tofauti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top