#VIDEO; Dr Biteko Avunja ukimya Asema Dunia inashuhudia yanayoendelea Tanzania

Adimin
0

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Dunia nzima imeshuhudia umahiri wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na uwepo wa mafanikio makubwa katika Serikali ya awamu ya Sita.


“Sisimizi alipanda begani kwa tembo, wakati tembo akivuka daraja la miti. Wakati tembo akipita juu ya daraja kwa uzito wake, daraja lilitikisika sana. Sisimizi akiwa begani kwa Tembo alijua daraja linatikisika lakini hakujua ni mtikisiko wa kiwango gani. Tembo aliporuka nga’ambo ya pili, sisimizi alisogea sikioni k7wa tembo akamwambia, ndugu tembo, mimi na wewe tumelitikisa daraja”. @biteko

“ Vilevile, Serikali imeendelea kuimarisha demokrasia, utawala bora na haki za binadamu kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na hivyo kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari ili kuwezesha wananchi kupata habari kwa wakati,” amesema Dkt. Biteko.
TAZAMA VIDEO YA DR BITEKO HII HAPA

Dkt. Biteko amesema hayo Mei 29, 2025 wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa - 2025 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top