Wajumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA iliyomaliza muda wake akiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara Benson Kigaila, aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, Catherine Ruge , John Mrema wametangaza kujiondoa CHADEMA kuanzia leo May 07,2025.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo akiwa ameambatana na wenzake hao, Kigaila amesema “Sisi tumeamua wote pamoja tunajiondoa CHADEMA ili tuwaachie hicho Chama waendeshe wanavyotaka, sisi hatuwezi kuwa Wanachama wa Chama ambacho maamuzi yake hayafanywi kwa vikao, hatuwezi kuwa Wanachama ambao Wanachama wanabaguliwa, Katiba haifuatwi, sisi sio chawa sisi tunajitambua, tuliingia CHADEMA kwa malengo na tunatoka CHADEMA kwasababu malengo yameisha basi tunawaaachia Chama chao”
“Nisiwaache mkaja kuniuliza maswali kwamba sasa mnaenda Chama gani kwasababu kuna fununu nyingi sana, sisi sio Wazee wakufikia kwenye kusahau, sisi bado tuna nguvu na malengo ya kisiasa, kazi ya kuwapigania Watanzania haijakamilika tutaendelea kuwapigania Watanzania waweze kufikia mahali ambapo CHADEMA ilikuwa inalenga na tutaendelea kupambana na CCM lakini tutatafuta jukwaa mwafaka”
👉👉CLIK VIDEO HAPA👈👈
“CCM haiwezi kuwa option yetu, tutatafuta jukwaa mwafaka ambalo tutakwenda tukahakikishe kazi ya kupigania haki, uhuru na maendeleo ya Watu inaendelea, tunaondoka leo CHADEMA tutashauriana na Vyama mbalimbali tutawaambia baadaye tunakwenda wapi?” —— Benson Kigaila