VIDEO; Mbunge Tarimba Aomba Mungu Amlaani Askofu Gwajibu 'Hana Shukrani'

Adimin
0

 Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mhe. Abbas Tarimba, amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kumchukulia hatua za Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima, kupitia Kamati ya Maadili ya chama hicho, kufuatia kauli alizotoa dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2025/2026,  Mei 26, 2025, bungeni jijini Dodoma, Mhe. Tarimba amesema kauli za Gwajima kuhusu madai ya utekaji ni za kudhalilisha na hazikubaliki, hasa pale zinapogusa familia ya Rais.

“Naiuliza CCM, huyu mtu bado ana kadi ya chama chetu, kwa nini awe huru kuendelea kutoa maneno ya fedheha kwa Rais wetu? Anatoa mifano ya kutisha, ya kumkosea heshima Rais na familia yake. Unamtaja mtoto wa Rais, ukisema atobolewe macho, hivi kweli unaelewa uchungu wa mzazi?” amehoji Tarimba.
TAZAMA VIDEO YA MBUNGE TARIMBA BUNGENI
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top