Klabu ya Yanga imemtaka Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao ajiuzulu, CEO wa Bodi ya Ligi TPLB, Almasi Kasongo ajiuzulu, Yanga pia imetaka Bodi ya uendeshaji wa ligi ivunjwe na Bodi ya Ligi TPLB iwe huru.
🗣"Wenzetu Yanga SC wamekuja na matakwa ya mambo manne na mambo hayo ni kuvunja kwa kamati ya uendeshaji wa bodi ya ligi (masaa 72), Kujiuzulu kwa Afisa mtendaji mkuu wa Bodi, Kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa TFF na Bodi ya ligi iwe huru."- Almasi Kasongo CEO TPLB.
Haya ndio Matakwa ya Yanga ili Derby Ichezwe
1- Kamati ya Masaa 72 yote ivunjwe.
2- Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu ajiuzulu.
3- Katibu Mkuu wa TFF ajiuzulu.
4- Bodi ya Ligi rasmi ibadili muundo na iwe chombo huru na sio sehemu ya TFF.
Bodi imeyapokea na imekiri kuwa yapo nje ya uwezo wao hivyo wanapeleka kwenye chombo husika.