Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza majina ya waamuzi watakaosimamia mchezo wa watani wa jadi, Yanga SC dhidi ya Simba SC, utakaopigwa Jumatano, Juni 25, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo namba 184 utaamuliwa na waamuzi kutoka Misri ambapo Mwamuzi wa kati ni Amin Mohamed Amin Omar (Misri), mwamuzi msaidizi wa kwanza Mahmoud Ahmed Abo El Regal (Misri), Mwamuzi Msaidizi wa pili Samir Gamal Saad Mohamed (Misri), Mwamuzi wa akiba ni Ahmed Mahrous Elghandour (Misri), Kamishna wa mechi Salim Omary Singano (Tanga, Tanzania) na Mkaguzi wa waamuzi ni Alli Mohamed (Somalia).