Balaa baadhi ya wanawake wa Pugu wazaa na waume za watu kupata Mali

Adimin
0

Timu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia wilayani Ilala imebaini katika Kata ya Pugu baadhi ya wanawake wanazaa na waume za watu na kujihesabia haki kuwa nao ni wake halali ilihali ndoa ya awali ya mwanaume huyo haijavunjwa kisheria.


Hivyo mwito wao ni kuwa elimu iendelee kutolewa kwa wananchi ili wawe na ufahamu wa sheria ya ndoa na kutojihusisha na waume za watu kwa sababu ni kosa kisheria, lakini pia ni jambo lisilo na maadili katika jamii na linachangia uwepo wa migogoro isiyo na sababu za msingi.

Hayo yalibainishwa na Mratibu wa kampeni hiyo wilayani Ilala, Dk Baraka Mkami alipozungumza na HabariLEO kuhusu tathmini ya kampeni hiyo katika Kata ya Pugu ambayo ni moja ya kata 10 za Wilaya ya Ilala zilizolengwa wananchi wake wafikiwe na huduma hiyo inayotolewa bure.

“Tumebaini huku (Pugu) wanawake wengi wanazaa na waume za watu ambao wamefunga ndoa za Kikristo, na hao wanawake (hawara) wanajihesabia haki, wanapita kifua mbele hawana hadhari ilihali ni kosa kisheria,” alisema Dk Mkami.

Alisema ndoa ya kikristo ni ya mke mmoja na kuwa ili mwanaume aliyeoa ndoa hiyo aweze kuoa mwanamke mwingine ni lazima ndoa ya awali ivunjwe mahakamani kwa takala kutolewa, baada ya mahakama kupitia shauri husika na kujiridhisha na madai yaliyowasilishwa.

“Jamii ina changamoto na tatizo kubwa ni elimu, wanadhani mume kutengana na mkewe waliyefunga nae ndoa ya kikristo ndio kuachana na kuwa anaweza kuoa. Hapana, lazima kama shauri lifike mahakamani la kutaka kuivunja hiyo ndoa na lisikilizwe na kama lina mashiko ndio mahakama inafanya uamuzi na takala inatolewa,” alisema Dk Mkami.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
To Top