Mganga wa Matunguli Jela kwa Kumbaka Mtoto

Adimin
0

Mahakama ya Wilaya Mkuranga Mkoa wa Pwani,Juni 24, imemuhukumu kifungo cha maisha jela Hemed Issa Kilindo (20) mganga wa kienyeji na mkazi wa Kitongoji cha Kitonombe, Tengerea wilaya Mkuranga kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la kwanza, miaka (9).


Mahakama imeeleza kuwa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho Novemba 11, 2024 huko Kijiji cha Tengerea Wilaya Mkuranga.

Baada ya shauri kusikilizwa mpaka mwisho kwa upande wa mashtaka na kuwaleta mahakamani mashahidi 7 shtaka lilithibitishwa pasi kuacha shaka na mshtakiwa alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
To Top