Kuelekea mchezo wa Kariakoo dabi Jumatano ya Juni 25,2025 (kesho) Kikanuni Simba na Yanga zilitakiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari leo ili kuelezea maandalizi na mambo mengine kuhusu mechi yao
Wenyeji wa mchezo Yanga SC wao wamefika na kufanya mazungumzo lakini Katika hali isiyo ya kawaida Simba SC hawajafika eneo ambalo mkutano ulipangwa kufanyika na jitihada za kuwatafuta zimegonga mwamba hivyo mkutano huo umeahirishwa ili kuendelea na ratiba zingine
“Simba walitakiwa kufanya mahojiano saa 5:30 asubuhi lakini hawajafika na tumejaribu kuwatafuta kwenye simu hawapatikani “ amesema Afisa habari wa Bodi ya Ligi Karim Boimanda wakati anaahirisha mkutano huo
See Translation