Mwanamke aliyeolewa jijini Nairobi nchini Kenya amezua mjadala mkali baada ya kukiri kuwa mumewe anawalea watoto wao watatu, ambao sio wa kwake huku akidhani kuwa wote ni wanawe.
Mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa ameyabainisha hayo wakati wa mahojiano na redio Maina Kageni, ambapo amefichua kuwa watoto wake wote watatu kila mmoaja ana baba yake, na kwamba sababu pekee ya yeye kukaa na mumewe ni utajiri na alikuwa akiwatunza.
“Kila mtoto ana baba yake na vyeti viwili vya kuzaliwa, ndiyo nimeolewa, kila mtoto cheti halisi cha kuzaliwa kipo kwa baba yake mzazi, mume ana hizo feki, yeye sio aina ambayo unapaswa kuzaa naye, ana pesa na si mtu ambaye alisoma shule na kupata fedha, ni bubu lakini aliingia kwenye biashara na kufaulu,” alisema.