Mwanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora (TABORA GIRLS) ambaye jina lake limehifadhiwa amejifungua Mtoto na kisha kumtelekeza kwenye Vyoo vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete ambapo alikwenda Hospitali hapo kupatiwa matibabu ambapo alidaia kuumwa na Mguu na Kichwa huku Wazazi pamoja na Walimu wakiwa hawafahamu juu ya ujauzito huo.
Akitoa taarifa ya tukio hilo Katibu Tawala wa mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya alipowasili shuleni hapo wakiwa wameongozana na kamati ya Usalama ya Mkoa amesema kuwa Mwanafunzi huyo alienda Hospitali kwaajili ya vipimo ambapo Madaktari walimwambia akalete Mkojo kwaajili ya vipimo na alipofika Chooni alijifungua na kumtelekeza mtoto Chooni.
VIDEO YAKE HII HAPA BOFYA
Baada ya watu aliokuwa ameongozana nao Hospitali hapo kugundua amechelewa kurudi ndio walipoenda Chooni na kusikia mtoto akilia akiwa ametelekezwa walimchukua na kumpeleka kwenye Uongozi wa Hospitali na baada ya uchunguzi kufanyika iligundulika Mwanafunzi huyo ndiye aliyemzaa na jitihada za kuokoa uhai wa mtoto yule zilianza na kufanikiwa
Mkuu wa mkoa wa Tabora Paulo Chacha ameelaani kitendo cha Uzembe kilichofanywa na Walimu na Madaktari wa kutomgundua Mwanafunzi juu ya ujauzito huo, huku amkiamuru Walimu walio tumika zaidi ya miaka kumi shuleni hapo kuhamishwa vituo vya kazi kwani wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea hali inayotajwa kuhatarisha ustawi wa Maendeleo ya Wanafunzi shuleni hapo.