Serikali ya awamu ya sita imeridhi pia madeni ya serikali zilizopita

Adimin
0

 Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa deni la serikali ni kutokana na fedha ambazo zilikopwa na awamu zilizopita kupokelewa na awamu hii ya sita.



Akilihutubia Bunge juni 27 Rais Samia amesema “Ni vyema tukafahamu kuwa mkopo unaweza kusainiwa leo lakini fedha husika zikaanza kupokelewa baada ya maandalizi ya mradi kukamilika na mradi kuanza ili lile deni au mkopo huo uingie kwenye deni la serikali lazima serikali iwe imepokea fedha hizo huduma au vifaa tulivyokubaliana”

“Katika awamu ya sita pamoja na kusaini mikopo mipya lakini pia tumeendelea kupokea fedha za mikopo ambayo ilisainiwa katika vipindi tofauti na kuongeza kiwango cha deni la serikali”

Rais Samia amesema serikali imepokea kiasi cha shiilingi Trilioni 11.3 ikiwa ni mikopo iliyosainiwa na awamu zilizopita.

Pamoja na hayo ameeleza pia sababu zingine ni kuimarika kwa dola ya Marekani jambo linalochangia kukua kwa deni la nje.

“mfano mwezi machi 2021 kiwango cha kubadilisha shilingi ya kitanzania dhidi ya dola za Marekani ilikuwa shilingi 2298.5 wakati mwezi Machi mwaka huu kiwango hicho kulikuwa 2650 hivyo endapo deni la serikali litatajwa kwa shilingi za Tanzania lazima lionekane limeongezeka”

Rais Samia ameeleza kwa sasa deni limeongezeka kwa zaidi shilingi trilioni 3.9 kutokana na ‘exchange rate’.

Hadi kufikia mei 2025 deni la serikali limefikia trilioni 107.7 ambapo deni la nje ni shilingi trilioni 72.94 na deni la ndani ni 34.76.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
To Top