Serikali yakiri Mikoa yenye Baridi Polisi wanapewa makoti kujilinda na baridi

Adimin
0

Serikali imesema makoti ya kujikinga na baridi ni miongoni mwa sare za Jeshi la Polisi, ambazo askari Polisi wanaofanya kazi kwenye mikoa yenye hali ya hewa ya baridi kali hupewa.



Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Suma Fyandomo, aliyehoji ni lini serikali itawapa makoti ya kujikinga na baridi askari polisi wanaofanya kazi katika mkoa wa Mbeya.

“Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa ambayo askari polisi wanapewa makoti ya kujikinga na baridi kali wakiwa kazini kama sare ya Jeshi la Polisi.

“Mikoa mingine inayopewa makoti ya kujikinga na baridi ni Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Wilaya ya Lushoto katika Mkoa wa Tanga,” amesema Naibu Waziri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top