Uongozi wa Klabu ya Young Africans umeweka wazi kuwa hautashiriki katika mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Simba SC, uliopangwa kufanyika Juni 15, 2025, hadi hapo matakwa yao yatakapotekelezwa.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa Juni 9, 2025, klabu hiyo imethibitisha kuhudhuria kikao maalum kilichoitishwa na Bodi ya Ligi Kuu kujadili mustakabali wa mchezo huo ambapo waliwasilisha msimamo wao kwa maandishi.