Siasa za CHADEMA na CHAUMA kiza nene wanafinishana

Adimin
0

 Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA, Kanda ya Kati, Jackson Jingu, amevitaka vyama vya siasa kufanya siasa za kistaarabu kwa kueleza sera kwa wananchi badala ya kufitinishana hali inayoweza kusababisha kuvunjika kwa amani na utulivu nchini.



Akizungumza na waandishi wa habari 7 juni 2025 amesema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa kuchagua Rais,wabunge na madiwani kunahitajika kuendesha siasa nzuri kwa kuelezea sera ambazo zitaweza kushawishi wananchi kukichagua chama husika.

"Siasa wanazofanya hivi sasa Chadema na Chaumma wanafitinishana hawaelezi sera za vyama vyao haya mambo hayana afya kwa taifa na yakiachwa kimsingi yanaweza kusababisha kuvunjika kwa amani" amesema Jingu ambaye alisema bado anatafakari chama cha kujiunga nacho baada ya kuachana na Chadema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top