Mwl atuhumiwa kwa kupenzika na Mwanafunzi Njombe

Adimin
0

 Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Mbembe iliyopo kata ya Wanging'ombe mkoani Njombe wameitaka serikali kuchunguza tuhuma za mwalimu mmoja ambaye jina lake halijafahamika ndani ya shule hiyo kwa kujihusisha kimapenzi na wanafunzi.


Wakizungumza na Mtandao huu baadhi ya wazazi wamesema kutokana na uwepo wa tuhuma hizo, mwalimu huyo hajaonekana tena kwenye kituo chake cha kazi,hivyo kuna haja ya serikali kufuatilia tuhuma hizo ili kama zina ukweli mhusika achukuliwe hatua.

Wazazi hao,Grayson Mpozi,Hezroni Luvata na Heri kikoti wamesema katika kipindi cha wiki mbili kuna mwanafunzi wa darasa la saba alibainika kuwa ujauzito mara baada ya vipimo vya awali zahanati ya katenge ambao alidaiwa kupewa na mwalimu huyo lakini walipopima mara ya pili hakukutwa na ujauzito huo.

Mzazi wa mtoto anayedaiwa kupewa ujauzito na mwalimu huyo amekiri kuwa aliitwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi mbembe na kuelezwa kuwa mtoto wake ni mjamzito lakini mara baada ya vipimo vya pili mtoto wake hakukutwa na ujauzitto na kueleza kuwa kwa kuwa mtoto wake amekiri kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwalimu huyo iko haja ya serikali kuchunguza tuhuma hizo.

Mwanafunzi huyo wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 14 amekiri kufanyiwa tendo hilo na mwalimu huyo na kueleza kuwa kabla ya tukio aliulizwa kama anaweza kutuza siri na tukio lilifanyika kwenye ofisi za walimu.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mbembe Issa Mtenda amesema licha ya mwanafunzi huyo kutopatikana na ujauzito mara baada ya vipimo vya pili bado mwalimu huyo anatakiwa kuchunguzwa kwa tuhuma za kutembea na mwanafunzoi na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni kweli anatabia hizo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top