"Kuanzia kesho tarehe mbili mwezi wa sita, tutaanza maombi ya kufunga na kuomba. Makanisa yote zaidi ya 2000 hata wale ambao si Ufufuo na uzima, wale ambao wanalipenda Taifa, kila mtu kwa dini yake, hata ndugu zetu Waislamu kila mtu kwa dini yake tutafunga na kuomba.
Aina ya maombi haya tutakunywa maji tu jioni, tutahudhuria hapa kuomba kwa muda wa siku saba,Tutaombea mambo gani? Jambo la kwanza tutaombea haki iendelee kutawala katika nchi ya Tanzania, Jambo la pili tutamuombe Mwenyekiti wa Chadema ambaye anashtakiwa kwa kesi ya uhaini, tutaendelea kumuombea kwa wiki nzima ili Mungu atende jambo.
Jambo jingine tutaombea viongozi wa kisiasa nchi nzima, sisi hatuangalii Chama cha mtu, sura ya mtu, sisi tunapenda Taifa likae kwa amani na ustawi.
FULL VIDEO YA GWAJIMA HII HAPA
Tutamuombea Mhe Zitto Kabwe,Kiongozu wa ACT, nampenda sana, wakati wa msiba wa Mama yangu pamoja na kwamba yeye ni muislamu, alihudhuria msibani kumzika mama yangu na Chama chake, tutamuombea pia Ibrahim Lipumba,ambaye ni kiongozi wa CUF, tutaombea vyama vyote vya upinzani.
Tutaombea pia Chama cha Mapinduzi,ambacho ndiyo Chama changu, tutaombea Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mama Samia Suluhu Hassan."- Askofu Josephat Gwajima wa kanisa na Ufufuo na uzima leo Juni Mosi kwenye ibada ya Jumapili.