Juni 1, 2025, baada ya mkutano wa hadhara Tanga Mjini, viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara John Heche, na Katibu Mkuu John Mnyika wametembelea nyumbani kwa Mzee Ali Mohammed Kibao kwa ajili ya kusalimia familia.
![]() |
Pichani ni mjane wa Mzee Ali Kibao akilia kwa uchungu |
Mzee Ali Mohammed Kibao, aliyekuwa kada wa chama hicho alikutwa ameuawa na kutupwa eneo la Ununio Jijini Dar es Salaam mwezi Septemba mwaka 2024 baada ya kutekwa kwenye basi kipindi akiwa safirini kuelekea mkoani Tanga.
HOTUBA YA JOHN HECHE AKIWA TANGA LEO