VIDEO; Bundi azidi kumzingira Askofu Gwajima,hali yazidi kudoda

Adimin
0

 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima amesema kuwa polisi wenye magari matatu wamezingira kanisa lake eneo la Ubungo Maziwa,Dar es Salaam majira ya saa 11:15 usiku wa Juni 2,2025.


Video aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram inamuonyesha akiwa na maaskofu zaidi ya saba huku akieleza kuwa wapo ndani na kanisa limezingirwa.
TAZAMA VIDEO HII YA GWAJIMA KANISANI

"Maaskofu wamekuja kusikiliza nini kinaendelea,mimi mwenyewe sijui nini kinaendelea ila hapo nje naona kuna defender za polisi kama tatu,wamekuja kuzunguka kanisa,hatujajua nini kinaendelea kwa hiyo tunataka maaskofu, wachungaji wetu wote na waumini mjue kwamba usiku huu tumezungukwa na polisi,sijui wanataka kufanya nini...hatujajua ni polisi au ni watekaji wenyewe,lakini hawa ni polisi,"amesema Gwajima ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top