VIDEO; Mahakama Kisutu Yamuonya Tundu Lissu, Asijaribu Kuidharau Mahakama tena

Adimin
0

 Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Wakili Tundu Lissu imeendelea tena  Jumatatu Juni 02.2025 kwa ajili ya kutajwa


Tofauti na ilivyofikiriwa hapo awali kwamba pengine shauri hilo lingechukua muda mchache kwakuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina nguvu ya kisheria ya kusikiliza shauri hilo, badala yake imeshuhudiwa mvutano 'mkali' wa kisheria baina ya Mawakili wa pande zote mbili

Jamhuri/ Serikali kupitia Mawakili wake ilianza kwa kuieleza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo kuomba Mahakama kuhairisha hadi siku nyingine, hata hivyo Jamhuri ilileta jambo lingine kwamba mtuhumiwa ameidharau Mahakama hiyo kwani wakati anaingia Mahakamani alitoa maneno (ya 'No Reforms, No Election') jambo ambalo ni kinyume cha sheria
VIDEO YA TUKIO HILO TAZAMA HII
Baada ya hoja hizo za Jamhuri, Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Mpale Mpoki, Dkt. Rugemeleza Nshala, Peter Kibatala na wengineo walipinga vikali na kuiomba Mahakama kufuta shauri hilo kwakuwa Jamhuri imeshindwa kukamilisha upelelezi kwa wakati, na kwamba kitendo cha kuchelewesha upelelezi ni kumnyima mtuhumiwa haki zake za msingi ikizingatiwa kuwa kupitia shauri hilo mtuhumiwa hawezi kujibu chochote

Kuhusu suala la mtuhumiwa kutoa maneno wakati anaingia Mahakamani, Mawakili wake wameileza Mahakama kuwa mtuhumiwa alicheleweshwa kuingizwa kwenye chumba cha Mahakama kwani ameingizwa kwenye chumba hicho sambamba na wakati Hakimu wa kesi husika anaingia, jambo ambalo limemkosesha mtuhumiwa uhuru wa kusalimiana na ndugu, jamaa na marafiki zake waliofika kumuunga mkono

Akitoa maamuzi, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu anayesikiliza shauri hilo amesema kwa mujibu wa sheria Mahakama inaanza tu pale Hakimu anapokuwa ameingia kwenye chumba cha Mahakama na kwamba kiutaratibu mtuhumiwa anapaswa kuingizwa kwenye chumba cha Mahakama baada ya Mahakama kuanza (yaani baada ya kesi husika kuitwa) na si vinginevyo, hivyo kutoa maelekezo kuwa utaratibu huo ndio unaopaswa kufuatwa hata itakapotajwa kwa wakati mwingine

Kuhusu suala la kutoa maneno wakati Mahakama imeanza, Hakimu amekubaliana na hoja za Jamhuri kuwa ni kweli mtuhumiwa ameidharau
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top