Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo nchini Tanzania CCT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo amesema kuwa baadhi ya watu kwa sababu zao binafsi wamekuwa wakidai kuwa msaada wa Rais, Dkt. Samia ni sehemu ya hongo, madai ambayo yamekuwa yakimuumiza sana kama kiongozi wa dini.
"Niendelee kumsihi Rais Samia asirudishwe nyuma na watu hao bali aendelee kuwa na hofu ya Mungu katika kusaidia huduma za kiroho nchini."
Askofu Mkuu Shoo amebainisha hayo Julai 03, 2025 Jijini Dodoma wakati wa Mkutano Mkuu wa 32 wa CCT ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano huo.
"Mahali pengine tunahitaji hekima, tunahitaji uelewa mzuri, tusifanye tu kama kuna sababu ya kumpinga Rais kwa namna yoyote ile, kumchukia kwasababu zako mwenyewe, kwa hiyo naomba Rais kwa unyenyekevu wake na kwa hofu yake anapotoa mchango kwa kazi ya kuwahudumia watu wa Mungu naomba sana tukwepe makosa makubwa ya kumsingizia kitu ambacho hajadhamiria kwenye moyo wake kwamba hii sasa ni rushwa." amesema Askofu Shoo