Soka la Kishirikina Lafika China: Changchun Xidu Yatuhumiwa Kuloga Mechi kwa 'Amri ya Kifalme'"

Adimin
0

 Katika soka la Afrika, matumizi ya imani za kishirikina si jambo geni ambapo matukio hayo yanatokea mara kwa mara na Watazamaji wamewahi kushuhudia magolikipa wakinyunyizia maji ya kiiman kwenye goli, wachezaji wakivaa hirizi au makocha wakibeba vitu visivyo vya kawaida kwa imani kuwa vitawasaidia kushinda mechi, Sasa hali hiyo imehamia mbali zaidi hadi nchini China.


Klabu ya Changchun Xidu FC, inayocheza Ligi Daraja la Tatu ya China imepigwa faini ya yuan 30,000 (zaidi ya shilingi milioni 13 za Kitanzania) kwa kutumia ushirikina dhidi ya timu pinzani kabla ya mechi yao wikiendi iliyopita.

Kabla ya kucheza dhidi ya timu ya Shanxi Chongde Ronghai, timu hiyo ilikamatwa ikiwa imeweka karatasi maalum za kiimani zinazojulikana nchini China kama fu kwenye chumba cha wachezaji wa wapinzani na karatasi hizo ni za imani ya Kidao (Taoism) na huandikwa kwa maandishi yanayoaminika kuwa na nguvu za kiroho aidha kwa bahati nzuri au kuleta mikosi, inaelezwa katika karatasi hizo, maandishi yalisomeka “Kwa amri ya kifalme, Shanxi Chongde Ronghai watashindwa.”

Changchun walishinda mechi hiyo kwa mabao 2-0 lakini baada ya tukio hilo kufichuliwa, Shirikisho la Soka la China (CFA) limesema ushindi huo unatia doa heshima ya mchezo pia Viongozi wa ligi hiyo wamesema kuwa si mara ya kwanza Changchun Xidu wanahusishwa na visa kama hivyo kwani tayari vilisharipotiwa na timu nyingine pia.

Aidha Shirikisho hilo limeeleza kuwa hatua hiyo ni ya awali tu na watachukua adhabu kali zaidi kwa yeyote atakayehusisha soka na imani za kishirikina kwa kuwa jambo hilo linavunja sheria na maadili ya michezo.

Vilevile tukio hili linakumbusha tukio jingine mwaka 2017 ambapo klabu ya Henan Jianye, iliyoonekana kuteremka daraja kwenye ligi kuu ya China iliwaalika makuhani 15 wa dini ya Taoist kufanyia uwanja wao tambiko maalum kabla ya mechi na kupelekea kushinda 2-1 na hatimaye wakafanikiwa kubaki kwenye ligi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top