Simanzi Pwani: Amkatakata Mpenzi Wake, Kisha Atimka DSM Kabla ya Kukamatwa!

Adimin
0

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Isaya Kastam, mkazi wa Simbani wilayani Kibaha, kwa tuhuma za mauaji ya kinyama dhidi ya mpenzi wake, baada ya kumkatakata kwa kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase, tukio hilo lilitokea saa nne usiku Julai 7 nyumbani kwa marehemu, ambapo mtuhumiwa alitoroka mara baada ya tukio na kukimbilia jijini Dar es Salaam, lakini baadaye alikamatwa.

Timu ya Wasafi Media ilifika nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Simbani na kuzungumza na baadhi ya ndugu na majirani. Anna Njavike na Fatma Omari walilaani vikali tukio hilo, wakilitaja kuwa la kikatili na kuomba vyombo vya ulinzi na usalama kumchukulia hatua kali mtuhumiwa kwa mujibu wa sheria, ili iwe fundisho kwa wengine.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Simbani, Nasra Madenge, alisema tukio hilo limewaumiza wakazi wa eneo hilo na kutoa wito kwa mamlaka kuchukua hatua stahiki dhidi ya mtuhumiwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top