Viongozi wa kata ya Ruhuhu maisha yao yapo shakani,,,wapokea vitisho kwa wasiojulikana

Adimin
0

Watu wasio julikana wamesambaza barua za vitisho ofisi mbalimbali katika kata ya Ruhuhu wilayani Ludewa, mkoani Njombe usiku wa kuamkia Disemba 03, 2024, na barua hizo zimeelekezwa kwa viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti aliyeapa siku chache zilizopita baada ya uchaguzi wa Novemba 27, 2024.


Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kata ya Ruhuhu barua nyingine imebandikwa imebandikwa ofisi ya Mtendaji kata ya Ruhuhu, ofisi ya mtendaji Kijiji wa kijiji cha Ngelelenge, ofisi ya chama Cha mapinduzi na  ofisi ya chama Cha ACT Wazalendo.


Barua hizo zimekuwa na ujumbe tofauti kwa kila mlengwa kwa  ofisi ya Mwenyekiti wa Kijiji ni "MARUFUKU KUINGIA HUMU MAANA HATUKUKUCHAGUA!"


Kwa Mtendaji wa Kijiji wameandika ni "NA WEWE MTENDAJI WA KIJIJI UKITAKA KUINGIA HUMU JIKANE
NAFSI YAKO NDIPO UINGIE HUMU!".

Katika ofisi ya Mtendaji kata wameandika "UMETUIBIA SANA TUMECHOKA KUVUMILIA NA SASA HIVI TUNAKWAMBIA KUTEMBEA KWAKO MWISHO SAA 12 JIONI JIADHARI MWISHO MUDA HUO. ULIPO UPO NA SISI MDA WOTE UTAKACHO KIPATA UTAKIJUA MWENYEWE".

Katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameandika barua inasema "TUMEVUMILIA TUMECHOKA MADUDE YENU MNAYO FANYA TUNAOMBA MTUPISHE HATA SISI VIJANA TUPO HAPA TUNAWEZA KUONGOZA".

Katika Ofisi ya ACT Wazalendo wakabandika barua isemayo "TUNAOMBA ENDELEENI KUKAZA HIVOHIVO" msipo kaza na nyie mkilegeza tutawaweka kwenye kundi moja la wale wajinga tulio waandika Barua.

Kings Fm (@kingsfmradio) imezungumza na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngelenge Joseph Mapunda (CCM) kata ya Ruhuhu ambae ndiye alitangazwa mshindi katika uchaguzi uliopita amethibitisha kupokea vitisho hivyo na ameeleza kuwa tangu jana Disemba 03, 2024 hajafungua ofisi kwani anaogopa.

Amesema kuwa tayari ameripoti suala hilo kwa viongozi wake wa Chama na Jeshi la Polisi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Idawa Media Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top